Nyumbani > Katiba > Oxfam yazindua utafiti wa ushiriki wa Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015
IMG_5241

Shirika la Oxfam limezindua utafiti kuhusu ushiriki wa wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 nchini Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Hotel ya Double view iliyopo Sinza jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wawakilishi kutoka serikalini, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na waandishi wa habari.

IMG_5199

Akizungumza katika uzinduzi huo Prof. Ruth Meena ambaye ndiye mtafiti Mkuu wa utafiti huo alisema; “Wanawake ni wadau muhimu katika shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii zote. Idadi yao kama wapiga kura, wanachama wa vyama vya siasa na kama wazalishaji wanaoendeleza kizazi ni kubwa na haiwezi kupuuzwa.”

IMG_5188

Akielezea mbinu zilizotumika kufanya utafiti huo, Prof. Meena alisema utafiti ulitumia vyanzo viwili vya kupata taarifa ikiwemo uchambuzi wa makala mbalimbali zilizoandikwa na wanazuoni na watafiti katika eneo hili na pili kupitia njia ya simulizi na mahojiano na wadau wakuu wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, Tume ya uchaguzi, viongozi wa vyama vitatu, TAKUKURU, pamoja na watendaji kutoka serikali za mitaa.

Mahojiano na wadau hawa yalitupa picha ya tafsiri ya wadau husika kuhusu majukumu yao katika kuwezesha usawa wa jinsia katika mchakato wa uchaguzi.

IMG_5205

“Mwisho tulipata simulizi kutoka kwa wanawake walioshiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi kama wagombea katika nafasi ya urais na ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na waliowania nafasi za uwakilishi wa mabaraza ya Kata au miji.” Aliongezea Prof. Meena.

Simulizi hizi zilitupa shuhuda kuhusu fursa zilizopo zenye kuwezesha pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo wanaposhiriki kama wagombea wanawake wa nafasi mbalimbali za uchaguzi.

IMG_5194

Naye Rashida Shariff, Meneja wa kitengo cha Haki Jinsia kutoka Oxfam alisema Lengo la utafiti huo lilikuwa ni kupata taarifa za kuwezesha Oxfam kuimarisha na kuboresha mipango kazi yake ya baadaye inayolenga kuboresha elimu ya uraia ili kuwezesha wanawake washiriki kikamilifu kama wapiga kura, wagombea na wasimamizi katika mchakato wote wa uchaguzi.

Aidha malengo mahususi ya utafiti huo ni pamoja na;

  1. Kuongeza hamasa ya Watanzania katika kuelewa vipingamizi vinavyozuia wanawake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
  2. Kutumia taarifa itokanayo na utafiti katika kuwahamasisha wadau wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi, msajili wa Vyama vya siasa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na asasi zisizo za kiserikali kubuni mbinu mbadala za kuwezesha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi wa haki na huru.
  3. Kutoa mrejesho wa matokeo ya mafunzo ya mradi wa Fahamu, Ongea, Sikilizwa II.

IMG_5239

 

IMG_5209

Akichambua utafiti huo, Dr. Alexander Makulilo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam alisema utafiti huo ulianza kwa kuangalia tatizo la wanawake kutokushiriki katika uchaguzi Mkuu. Akifafanua Dr. Makulilo alisema tatizo hili sio la Tanzania peke yake bali ni la dunia nzima.

IMG_5227

 

IMG_5234

 

IMG_5225

IMG_5240

IMG_5223

 

Soma utafiti huu kwa Kiswahili kwa kubofya hapa na kwa Kiingereza kwa kubofya hapa

Kufahamu zaidi kuhusu mradi wa Fahamu Ongea Sikiliza tembelea ukurasa wake wa Facebook

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*